Luke 20

Swali Kuhusu Mamlaka Ya Isa

(Mathayo 21:23-27; Marko 11:27-33)

1 a bSiku moja, Isa alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wa watu wakamjia. 2 cWakamuuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

3Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. 4 dJe, ubatizo wa Yahya ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”

5Wakahojiana wao kwa wao wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 6 eLakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yahya alikuwa nabii.”

7Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.”

8Isa akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Mfano Wa Wapangaji Waovu

(Mathayo 21:33-46; Marko 12:1-12)

9 fAkaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 10 gWakati wa mavuno ulipofika, akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili wampe sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 11Akamtuma mtumishi mwingine, huyo naye wakampiga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. 12Bado akamtuma na mwingine wa tatu, huyu pia wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba.

13 h“Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa, huenda yeye watamheshimu.’

14“Lakini wale wapangaji walipomwona, wakasemezana wao kwa wao. Wakasema, ‘Huyu ndiye mrithi. Basi na tumuue ili urithi uwe wetu.’ 15Kwa hiyo wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.”

“Sasa basi yule mwenye shamba la mizabibu atawafanyia nini wapangaji hawa?
16 iAtakuja na kuwaua hao wapangaji, na kuwapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu.”

Watu waliposikia hayo wakasema, “Mungu apishie mbali jambo hili lisitokee!”

17 jLakini Isa akawakazia macho, akasema, “Basi ni nini maana ya yale yaliyoandikwa: “ ‘Jiwe walilolikataa waashi,
limekuwa jiwe kuu la pembeni’?

18 kKila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”

19 lWalimu wa sheria na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja, kwa sababu walifahamu kwamba amesema mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu.

Kumlipa Kaisari Kodi

(Mathayo 22:15-22; Marko 12:13-17)

20 mKwa hiyo wakawa wanamchunguza na kutuma wapelelezi waliojifanya kuwa wenye haki ili wapate kumtega kwa maneno asemayo, ili wamtie katika uwezo na mamlaka ya mtawala. 21 nHivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli. 22Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

23Lakini Isa akatambua hila yao, kwa hiyo akawaambia, 24“Nionyesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyoko juu yake ni vya nani?”

25 oWakamjibu, “Ni vya Kaisari.”

Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”

26Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza kimya.

Ufufuo Na Ndoa

(Mathayo 22:23-33; Marko 12:18-27)

27 pBaadhi ya Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa na kumuuliza, 28 q“Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. 29Basi palikuwepo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa, akafa bila kuzaa mtoto. 30Kisha yule wa pili akamwoa huyo mjane, naye akafa bila mtoto, 31naye wa tatu pia akamwoa. Vivyo hivyo ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mwanamke, na wote wakafa pasipo yeyote kupata mtoto. 32Mwishowe, yule mwanamke naye akafa. 33Sasa basi, siku ya ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?”

34Isa akawajibu, “Katika maisha haya watu huoa na kuolewa. 35 rLakini wale ambao wamehesabiwa kwamba wanastahili kupata nafasi katika ulimwengu ule na katika ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaolewi. 36 sHawa hawawezi kufa tena, kwa maana wao ni kama malaika. Wao ni watoto wa Mungu, kwa sababu ni watoto wa ufufuo. 37 tHata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Bwana, ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.’ 38 uYeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa kuwa kwake wote ni hai.”

39Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawasawa kabisa!”

40 vBaada ya hayo hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza maswali tena.

Al-Masihi Ni Mwana Wa Nani?

(Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37)

41 w xKisha Isa akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Al-Masihi
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
ni Mwana wa Daudi?
42 zDaudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,

43 aahadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’

44Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”

Isa Awashutumu Walimu Wa Sheria

(Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40)

45 abWakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Isa akawaambia wanafunzi wake, 46 ac“Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. 47 adWao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”
Copyright information for SwhKC